Yanga yaelekeza nguvu zake Ligi kuu
BAADA ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, Klabu ya Yanga imesema kuwa sasa hivi inaelekeza nguvu na akili zake kwenye michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ilimaliza michezo yake ya Kombe la Shirikisho kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na Rayon Sports katika mchezo wa kukamilisha ratiba uliofanyika juzi jijini Kigali, Rwanda.
Kwa njia ya simu jana, Meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro', alisema kuwa matokeo waliyoyapata Rwanda wanayaacha huko huko na wanarejea nchini wakielekeza silaha zao katika mechi za ligi kuu.
"Mchezo ulikuwa mgumu, lakini pia hali ya hewa haikuwa rafiki, lakini tuseme tu matokeo ya huku tunaachana nayo na kwa sasa nguvu zote ni kwenye ligi," alisema Cannavaro.
Alisema kuwa hawana kitu kingine cha kukiwazia zaidi ya michezo yao ya ligi kuu inayowasubiri.
"Hatuna kitu kingine kwa sasa zaidi ya ligi...kocha sasa anaelekeza mipango yake yote kwenye ligi, lengo kufanya vizuri na kurejesha ubingwa wetu," aliongeza.
Naye Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema kuwa wamerejea nchini jana mchana na leo kikosi cha timu hiyo kilichoko chini ya Kocha Mwinyi Zahera kitaendelea na programu yake ya mazoezi kwa ajili ya kuivaa Stand United.
Yanga yaelekeza nguvu zake Ligi kuu
Reviewed by kondoairangi
on
August 31, 2018
Rating: 5
No comments