Pata kufahamu kabila la Wasi linalopatikana Kondoa irangi
Wasi (au Waalagwa) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa, hasa tarafa ya Kolo katika vijiji kama Kwa Dinu, Mneniya, Hurui n.k. Kati ya makabila yaliyopo Kondoa linaweza kuwa kabila la pili kwa ukubwa na wingi baada ya Warangi.
Lugha yao ni Algwaisa si Chasi. Lugha hii si ya Kibantu, kwani huendana na Kifyomi, Kiiraqwa na Kiburunge. Kabila hili sehemu zote wanazokaa wenyewe huongea lugha hii na ndiyo asili yao ya wazazi wao waliowakuta
Katika taarafa ya Kolo kulikuwa na mmiliki aliyeitwa sultani Salim Kimolo (toka enzi za ukoloni). Sultani huyo alikuwa anaongea sana lugha hiyo, ukizingatia yeye alikuwa mtu kama jamii ya Wamang'ati au Wairaqw. Alipofika Kondoa - Kolo na lugha hiyo ilipochukua nafasi akapaita Kolo kama Kolowasi. Alikuwa na watoto 43, na watu wote walimuheshimu na kutumia lugha hiyo hata katika kutoa maamuzi wakati wa kesi mbalimbali. Watu wengi wa jamii hii ni Waislamu na ni kutokana na mahusiano kati ya sultani Salim Kimolo na Waarabu hapo zamani.
No comments