Ushauri maalumu kwa wanandoa juu ya matumizi ya fedha
Habari za muda huu mdau na mfuatiliaji wa makala mbalimbali kutoka hapa Muungwana Blog, kwa heshima na taadhima naomba nikualike rasmi hapa jamvini ili niweze kusema na wewe mwanandoa juu ya elimu na matumizi ya fedha pindi muwapo ndoani.
Nataka niseme na wewe kuhusu matumizi ya pesa kwenye suala la ndoa kwa sababu miongoni mwa migogoro mingi ya wanandoa wengi chanzo chake kikubwa huwa ni fedha.
Wengi wao wamekuwa hawana ushirikiano mzuri kuhusu namna ya kupata na namna ya kuzitumia pesa hasa wawapo ndoani.
Hili lipo wazi kwamba mwanaume ndiye kichwa cha familia, pesa anazotafuta mwanaume ndizo zitakazosaidia kutatua matatizo ya familia, ila pesa anazotafuta mwanamke basi hizo ni zake.
Kwa misingi hiyo siku mwanaume akimwambia mkewe hana hela, basi katika familia hiyo hapatakalika, hii ni kwa sababu ya ushirikiano finyu juu ya elimu sahihi ya pesa kwa wanandoa.
Hivyo ili kuweze kuwa na maelewano sahihi kwa wanandoa hususani katika kipengele cha pesa kunatakiwa kuwe na mambo yafuatayo;
1. Wanandoa ni lazima waelewe wao ni mwili mmoja hata katika suala la kifedha pia, hivyo wanatakiwa kupeana mawazo thabiti ya jinsi ya kupata na namna ya kuzitunza pesa wanazozipata, na si kuzitunza tu hata kuzifanya ziweze kujizalisha zenyewe.
2. Ewe mwanamke, Maisha yenu yanakuwa duni kwa sababu bado unaishi katika dhana na imani ya kizamani kwamba pesa zako ni zako tu, kwa misingi hii kama utaendelea kuibebeba basi neno ndoa thabiti utaendelea kuona kama hadithi tu hivyo ili uweze kuifurahia ndoa yako basi unatakiwa kuelewa kuwa pesa unazozipata kupitia shughuli mbalimbali unazozifanya pindi utakapoamua kumshirikisha mumeo basi ni lazima maendeleo makubwa yatakuwa upande wenu.
3. Wanandoa ni lazima wawe na utaratibu wa kuweka akiba, akiba ni muhimu katika ndoa kwa sababu pindi litakapotokea jambo ambalo halipo sawa /changamoto basi akiba hiyo itawasaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kutatua changamoto hiyo mara moja.
4. Pindi mnapojiingiza katika madeni kama vile mikopo basi wekeni jitihada za namna ambavyo mtashirikiana kulipa deni hilo, na si kumuachia mtu mmoja tu ashughulike na ulipaji wa madeni. Pia kumekuwako na hulka ya mwanaume kuchukua mkopo pasipo kumshirikisha mkewe, hii si tabia nzuri hata kidogo, ewe mwanaume pindi ukitaka kuchukua mkopo hakikisha unamshirikisha mkeo juu ya mkopo uliyouchukua.
Pindi ukiamua kuyazingitia hayo machache ambayo nimewaeleza kuhusua pesa ni kwamba maisha yenu ya ndoa yatakuwa ni maisha ambayo hayana migogoro ya mara kwa mara ambayo yatatokana na mambo ya kifedha pindi muwapo ndoani.
Na. Benson Chonya

Reviewed by kondoairangi
on
April 06, 2019
Rating: 5
No comments