Kocha Mbelgiji wa Simba kuleta Beki na Kiungo
KOCHA pande la mtu aliyemwaga wino Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amewaambia viongozi anataka wachezaji wengine wawili wa maana.
Timu hiyo hadi sasa imewasajili Meddie Kagere, Adam Salamba, Mohamed Rashid, Marcel Boniventure, Hassani Dilunga na Deogratius Munishi ‘Dida’ kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo baada ya kukiangalia kikosi hicho kwenye baadhi ya mechi za Kombe la Kagame ametoa baadhi ya mapendekezo ya usajili kwa kusajili beki na kiungo mwenye uzoefu kutoka nje ya nchi maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mtoa taarifa huyo alisema, Simba katika usajili wao wamebakisha nafasi mbili pekee za wachezaji wa kimataifa ambazo wamepanga kuzijaza kusajili beki na kiungo huyo.
Wachezaji hao Wakimataifa waliokuwepo ni James Kotei, Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Haruna Niyonzima, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, Pascal Wawa na Fabrice Mugheni.
“Uongozi ulipanga kubakisha nafasi hizo mbili za usajili wazi kwa ajili ya dirisha dogo, lakini kutokana na mahitaji ya kocha ambao aongezewe wachezaji wengine wawili wa kimataifa wenye uzoefu kutoka nje ya nchi.
“Anawataka wachezaji hao maalumu kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tutakayoshiriki mwakani na kikubwa kocha anataka kuhakikisha inafikisha Simba katika nafasi nzuri.
“Hivyo, wakati wowote wachezaji hao huenda wakatua nchini kwa ajili ya kukamirisha usajili huo baada ya kocha kuridhika nao,” alisema mtoa taarifa huyo.
Kaimu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ juzi katika utamburisho wa kocha huyo alisema kuwa: “Kocha amekiona kikosi chake katika michuano ya Kagame na kuona baadhi ya upungufu ambao anahitaji kuuboresha na tayari mapendekezo hayo ameyakabidhi kwa uongozi na hivi sasa tunafanyia kazi.”
Kocha Mbelgiji wa Simba kuleta Beki na Kiungo
Reviewed by kondoairangi
on
July 22, 2018
Rating: 5
No comments